Napenda tena kuchukua nafasi hii adimu kumshukuru
Mwenyezi Mungu muumba wa mbingu na nchi kwa kunipa nafasi ya kuwasilisha kwenu
baadhi ya mazoea mabaya ustawi ndoa ambayo hufanywa na wanandoa wengi. Pia
napenda kuwashukuru wale wote waliopata nafasi ya kusoma makala zangu kwa maoni
na mawazo yenu mazuri, napenda kuchukua nafasi hii kuwaombeni mwaalike na wenzenu
kusoma makala zangu ambazo huwa natoa kila wiki.
Leo nitaongelea makosa saba (7) ambayo mara nyinyi
hufanywa na wanandoa na kusababisha kuibuka kwa migogoro katika mahusiano.
Makosa hayo ni kama yafuatavyo: -
1.
Kususia
tendo la ndoa bila sababu ya msingi; Tendo la ndoa ni mmojawapo
wa nguzo muhimu ya ndoa zote. Kwa hiyo, inapotokea mmoja wa wanandoa kuamua
kumnyima mwenzake tendo la ndoa bila sababu ya msingi ni tendo ambalo linaweza
kusababisha kuvunjika kwa ndoa bila kujali ni ya kidini, kimila au kiserikali.
2.
Kumsema
vibaya mwenzako wako kwa rafiki/ndugu; Ni makosa makubwa sana kwa
mustakabali wa ndoa kwa mmoja wa wanandoa kumsema vibaya mwenzake kwa rafiki
zake au ndugu zake badala ya kumuelimisha ili kuondoa kasoro unazoziona kwake.
3.
Kutotimiza
yale unayosema; Ni kosa kubwa sana kwa mwanandoa
kutotimiza/kutenda yale anayoahidi kwa mkewe/mmewe bila sababu ya msingi. Katika
mahusiano hutokea misukosuko ya hapa na pale na nyingi hutokea mmoja wa
wanandoa kuomba msamaha na kukiri kutorudia vitendo fulani ambavyo ni kero kwa
mwenzako kwa mfano; kulala nje, kuchelewa kurudi nyumbani bila taarifa yo yote,
nakadhalika.
4.
Kutokukubali
makosa; Ni busara kwa mstakabali mzuri wa ndoa kukubali makosa
inapotokea kuwa mmoja wa wanandoa kafanya makosa. Imekuwa ni vigumu sana kwa
wanandoa hasa wanaume kukubali makosa inapotokea wamefanya makosa na badala
yake huonyesha kukiri kwa vitendo yaani; kufuata mapendekezo ya wake zao na siyo
kukubali kwamba maamuzi yao ya awali yalikuwa na makosa. Si dhambi kukiri
kufanya maamuzi kimakosa inapotokea kwa mustakabali mwema wa mahusiano.
5.
Kuwa
na hasira zisizo na mpangilio; Ni makosa makubwa kuwa na
hasira zisizo na mpangilio kwa mwenzako au kuhamisha hasira kutoka ofisini au
kwenye shughuli yo yote unayoifanya na kuzipeleka nyumbani.
Nyumbani
ni mahali ambapo inakiwa iwe ni pakupatia faraja na pumziko stahili.
6.
Kutojishughulisha
na kumuelewa mwenzako; Ni jambo jema kwa mustakabali mzuri
mahusiano kufanya jitihadi kumuelewa mwenzako anakuweje katika hali ya furaha
au huzuni. Hili ni muhimu sana katika mahusiano hata katika urafiki wa kawaida.
Hii ni nguzo muhimu sana katika kudumisha mahusiano kwa wanandoa. Kinyume cha
hapo ni kujenga mifarakano isiyo lazoma.
7.
Kutomshukuru
mwenzako anapokuwa amefanya jambo zuri; Ni vizuri inapotokea
mwanaume/mwanamke kafanya jambo jema kumshukuru ili kumpa moyo wa kufanya
vizuri zaidi siku nyingine. Kwa mfano kama mwanaume/mwanamke ameamua kwa upendo
kukununulia zaidi ya nguo ni busara kumshukuru kwanza kwa zawadi hiyo badala ya
kulaumiwa kwamba nguo hiyo siyo nzuri au imeshapitwa na wakati, umeuziwa bei
mbaya, karudishe nakadhalika.
Mambo yote hayo niliyoyataja hapo juu yanaweza kuepukwa, iwapo
utakuwa mtafiti na utamweka Mungu karibu katika maisha yako yote. Na pia kwa ushauri naomba tuwasilianae kwa
barua pepe ya fkmwamoto@gmail.com kwa ushauri makini wa masuala ya mahusiano.